NYUKI ANA FAIDA KUBWA KATIKA KILIMO-MAJENGO NYUKI


Wakulima wanatakiwa kufahamu thamani ya Nyuki katika kilimo namna anavyoweza kuchamvusha mimea ambapo kitalaamu asilimi 85 ya mazao anaweza kuyafanya yanawili vizuri zaidi.



Hayo ameyasema leo Mkulima na mfanyabiashara wa Nyuki Mohamed Juma maarufu kama Majengo Nyuki alipoongea na blogg hii juu ya darasa atakalolitoa siku ya Jumatatu ya tarehe nane ambapo ataelezea kilimo cha uchamvushaji pamoja na faida zake.

"Kwanza niwakaribishe wote wafike pae Manga siku ya Jumamosi wajionee namna Nyuki alivyokuwa  na faida," Majengo

Aidha ameweka wazi kuwa lengo la darasa hilo Mkulima ajue namna nyuki anavyoruka katika maua na atakavyotengeneza uchamvushaji wa mazao.

Majengo amesema kuwa nyuki hatengenszi asali pekee yake bali ana matumizi mengine kwa binadamu.

Majengo amesema kuwa ataendelea kutoa darsa hilo kwa watu mbalimbali ili wapate kufahamu thamani ya nyuki na wawafuge ili wafaidike katika biashara ya kilimo. 

Darasa hilo litafanyika siku ya Jumatatu kijiji cha Manga na elimi mbalimbali za nyuki na faida zake zitaelezwa Majengo anawakribisha wote. 

Mwisho


Post a Comment

Previous Post Next Post