KISHOA AWASHIKA MAMA NTILIE IBAGA




Mbunge wa Viti Maalumu Jesca Kishoa jana ametoa mitungi thelathini ya gesi kwa Mama Ntilie waliopo Kata ya Ibaga Wilaya ya Mkalama mkoani Singida ili ziwasaidie katika shughuli zao za kujitafutia maendeleo. 


Mbunge Kishoa amewaomba watu mbalimbali kuendelea kupambana katika kutafua rizk zao halali ndio maana amewiwa kutoa mitungi ya gesi huku akiahidi ataendelea kuwasaidia wajasiliamali wengine ili kuwakwamua pale ambapo wamepelea.


"Nitaendelea kutoa mitungi ya gesi kwa wengine ambao hamjapata siku nyingine niwapongeze kwa kuendelea kupambana sisi tupo nyuma yenu kuendelea kuhakikisha serikali inaendelea kuleta huduma nzuri ili mfanyekazi kwa amani," Kishoa.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwaahidi kutoa mitungi 98 ya gesi kwa shule za msingi na Sekondari ya Kata hiyo kwa ajili ya kusaidia matumizi yao ya shule hizo.


Kishao amewaambia ataendelea kuviunga mkono vikundi mbalimbali vya Wazee, Wakina Mama pamoja Walemavu ili vikue navifikie malengo yao kadri atakavyojaaliwa na Mungu.

Baada ya kumaliza kiako amewatembelea wajasiliamali wanaouza bidhaa ndogondogo magengeni na kuwaunga mkono huku akiwahimiza wasikate tamaa.

Kishoa amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuwalinda na kuwajali wananchi wake kwa kuweza kusimamia vyema miradi mbalimbali ya maendeleo, amesema kuwa namna Rais Samia anavyowajibika na kufungua njia kwa miradi ya maendeleo inawafanya wao wabunge pia wasilale ndio maana amemuunga mkono kwa kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo. 


"Nimpongeze Rais Samia kwa kuendelea kupambania nchi yetu, anachokifanya ndicho ambacho tunataka akifanye ili tuendelee kuishi katika ardhi iliyobora na bila vurugu," Amesema. 


Mwisho. 

Post a Comment

Previous Post Next Post