KISHOA AUNGA MKONO JITIHADA ZA SAMIA ATOA VIFAA VYA MICHEZO IBAGA

 


Katika kuunga mkono jitihada za Rais Dokta Samia Suluhu Hassan za maendeleo Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Jesca Kishoa jana ametoa vifaa vya michezo ikiwemo jezi seti 14 na mipira kwa timu za kata ya Ibaga ili ziendeleze vipaji vyao. 


Kishoa amesema ya kuwa anafurahi kuona Rais Samia akitoa hamasa mbalimbali katika michezo hii imemfanya naye kumuunga mkono kwa kutoa vitendeakazi kwa timu 14 za Ibaga ili waoneshe vipaji vyao ikiwezekana nawao waonekane katika timu kubwa na watengeneze ajira zao. 


"Nendelea kufurahishwa na Rais Samia kwa kuunga mkono michezo na mimi natumia fursa hiyo kuwapa leo jezi kwa timu 14 za kata ya Ibaga mkacheze mpira na muoneshe vipaji vyenu najua kuna watu watachukuliwa na timu mbalimbali na sisi Mkalama tukajivunia nao, "Amesema

Kishoa alifika Kata ya Ibaga ikiwa na lengo la kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa Bunge ikiwa na yeye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo haki na wajibu wa kuwaelezea wananchi wake kile kinachoendelea. 


Licha ya hayo ameshika mikono watu mbalimbali ambao wamefika katika mkutano huo amewatia moyo katika uoambanaji na kuwasihi wasichoke kutafuta wao kama wabunge wataendelea kuona njia gani nzuri ya kuwarahisishia katika shughuli zao kupitia huduma za kijamii. 

Mwisho. 

Post a Comment

Previous Post Next Post