KISHOA KUMALIZIA ZAHANATI YA KATA YA IBAGA


Zahanati ya IBAGA Wilaya ya Mkalama itaanza kutoa huduma hivi karibuni baada ya kuahidiwa kupatiwa fedha za ujenzi uliobaki wa kiasi cha shilingi milioni tatu na laki mbili ili kumalizia sehemu zilizobaki kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo.


Fedha hizo zimeahidiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Jesca Kishoa hapo jana alipofika nakuongea na wananachi wa  kata hiyo wakati anatoa taarifa ya utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Bunge.

Kishao amewapongeza Wananchi kwa Jitihda zao za ujenzi huo ambapo kwa nguvu zao walipofikia yeye amechukua jukumu la kuweza kuwaunga mkono ili waanze kupata huduma katika ardhi yao salama.

" Niwapongeze wananchi kwa jitihada zenu mnazoendelea kuzifanya kwa kuanzisha Zahanati kwa hatua mliyofikia nimeiona kwa macho yangu nimeambiwa imebakia kiasi shilingi milioni tatu na laki mbili kwa ajili ya kumalizia sehemu iliyobaki naichukua mimi hiyo iliyobaki, nitatoa pesa hizo ndani ya siku tatu ili imaliziwe na Zahanati hii ianze huduma mara moja," Kishoa 


Aidha katika hatua nyingine Kishoa katika mkutano huo wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali juu ya maeneo yao ikiwemo  Ukosefu wa Maji Safi, Barabara kutokuwa vizuri baadhi ya maeneo pamoja na kituo kimoja cha Afya kikongwe ambacho kimetelekezwa.

Kishoa amewaahidi juu ya Maji ataongea na Waziri wa Maji kuona namna gani wanaanza kuitatua shida hiyo, Barabara mbalimbali za eneo hilo ameahidi kuendelea kuzipeleka bungeni kama alivyoiongelea Barabara ya kutoka Iguguno hadi Nduguti ambapo Serikali wameahidi kuipatia fedha pia atafanya hivyo katika kero nyingine ili wananchi wapate huduma safi zinazoendana na maisha ya hivi sasa ya Sayansi na Teknolojia.


 "Niwaahidi ndugu zangu kero zenu nimezisikia na nyingine nimezioa nitazilepeka Bungeni ili zipatiwe ufumbuzi zaidi, juu ya hili la maji pia nitaongea na Waziri wa Maji ili tuone atatusaidiaje, " Kishoa. 

Lakini pia amemsaidia Mwananchi kwa jina maarufu la Mourinho aliyepata ajali ya gari kwa kumpatia nauli ya shilingi laki tano kwenda kupata matibabu katika hospital ya Makiungu baada ya kujielezea na alivyokuwa na uhitaji wa nauli kwa ajili ya kwenda kupata matibabu. 

Mwisho. 

Post a Comment

Previous Post Next Post