SMAUJATA SINGIDA WAPO TAYARI KWA SHUGHULI YAO KUBWA LEO



Uongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Singida ukiongozwa na Mwenyekiti Ambwene Kajula leo wametembelea kata ya Mwankoko kuona maandalizi ya shughuli itakayofanyika kesho kuanzia saa  tatu asubuhi.



Katika safari hiyo Mwenyekiti amepata nafasi ya kuongea na baadhi ya vijiwe kuhusu mkutano wa kesho lakini amepata nafasi ya kuongea nao juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia.


Ambwene amewaomba kusema yale wanayoyasumbua wanapokuwa majumbani pamoja na kutoa taarifa pindi maswala ya ukatili wanapoyaona au kuyasikia mahali.


"Nawaomba mtuambie mambo ya ukatili majumbani kwenu lengo letu kuona Tanzania inakuwa salama hakuna mambo ya ukatili Kila mtu aishi salama na ajitafutie rizk zake za kila siku," Ambwene


Baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo hilo wamefurahishwa na ujio wa SMAUJATA na kuahidi kushiriki huku wakisema kuwa watasema Kila kitu siku ya kesho.


Shughuli ya kuwahsukuru viongozi mbalimbali wakiwemo wa serikali na wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) pamoja na kupeana hamasa kwa mashujaa waendelee kuzuia na kukataza ukatili mkoa wa Singida.


Katika msafara huo Kajula ameambatana na Makamu Mwenyekiti Elineema Babu, Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaaa ya Singida Miraji Hamis, Mkuu wa Idara ya Habari Aminii Nyaungo pamoja na Katibu wa Idara ya Makundi Maalum Manispaaa ya Singida Hawa Ntandu. 


KATAA UKATILI WEWE NI SHUJAA

Post a Comment

Previous Post Next Post