Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Maulid Kiaratu amewaomba SMAUJATA mkoa wa Singida waendelee kusimamia haki na kuvumbua matatizo yanayoikabili familia mbalimbali nchini Tanzania.
Kiaratu ameyasema hayo jana Alhamis tarehe 28.03.2024 katika mkutano wa shukran ulioandaliwa na SMAUJATA Mkoa wa Singida uliofanyika kata ya Mwankoko Manispaa ya Singida mkoani Singida.
Amewapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya bila kuchoka kwa muda wote huku wakisaidia jamii kwa kukataza na kupambana na ukatili wa kijinsia.
Aidha Kiaratu amesema kuwa matukio manne ambayo ndio sababu ya mkutano huo naye ameshiriki akiwa kiongozi wa eneo husika, akiyataja matukio hayo juu ya mtoto Naifat Ayoub ambaye alizaliwa akiwa hana njia ya haja kubwa, Mtoto mwenye moyo mpana, Mtoto mwenyeshida ya Figo pamoja na mtoto aliyeungua moto mwili mzima.
"Niwaombe SMAUJATA muendelee kusaidia watu mbalimbali sisi viongozi tupo nyuma yenu mnafanyakazi nzuri sana," Yagi
Katika mkutano huo pia Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Sospeter Bulugu amewashukuru viongozi wa serikali waliojumuika pamoja huku akiwaomba jamii kuungana na SMAUJATA ili matendo hayo ya ukatili yaweze kukomeshwa.
"Niwashukuru kwa kuungana nasi siku hii ya leo, pia niwaombe tuungane kwa pamoja ili tutokomeze maswala mbalimbali ya ukatili, " Bulugu.
Naye Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Singida Ambwene Kajula yeye amewashukuru viongozi wa mkoa wa Singida kwa ushirikiano mzuri wanaounesha kwa jamii ya Tanzania huu akimpongeza Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu kampeni hiyo.
" Nawashukuru viongozi wa mkoa wa Singida kwa ushirikiano wenu lakini pia Rais Samia kwa kuruhusu kampeni hii," Kajula
Katika tukio hilo walikuwepo mashuhuda wanne walioweza kusaidiwa na SMAUJATA kuwaunganisha na wadau pamoja na serikali.
Mama Naifat mwenye mtoto ambaye alikuwa hana njia ya haja kubwa ametumia nafasi hiyo kuwashukuru SMAUJATA, Viongozi wa Serikali pamoja na Rais Samia kwa kutoa ushrikiano kwa mtoto wake kupata matibabu hadi amepona.
Kwa ujumla wake wote waliokuwepo wameshukuru SMAUJATA nakuahidi kuendelea kutoa ushirikiano na kuwaomba viongozi wa Serikali kutoa ushirikiano kwa SMAUJATA ili waweze kufika maeneo mengi ili wawasaidie wananchi.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Singida Elineema Babu aliwaomba wote walioshiriki zoezi hilo kuchangia fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao kupata bima ya afya ili iwasiaide mwaka mzima, na alianza kutoa harambee hiyo ambapo mwisho wa tukio ikapatikana kiasi cha shilingi laki moja na hamsini kwa ajili ya bima ya watoto hao.
Kwa upande wake Katibu wa SMAUJATA mkoa wa Singida Juma Maftah amewashukuru viongozi, wananchi na wote walio hudhuria tukio hilo na kutoa ushirikiano wa hali na mali.
*KATAA UKATILI WEWE NI SHUJAA.*
Post a Comment