Moja ya studio ambayo ilifanya vizuri zamani ni pamoja na Bongo Records wakati huo walikuwa wanashindana na Master Jay ilikuwa kivumbi sana.
Majani aliwakaribisha watu mbalimbali studioni kwake kuweka ufundi wao, mfano mzuri Bizzman alipiga vinanda katika ngoma nyingi za Bongo Records.
ALIKIMBIAJE STUDIO
Uliwahi kusikia ule msemo hata uchawi unazidiana?
Hilo ndio lililomtokea P Funk , hakuna anayebisha juu ya uhodari wake wa kuzalisha muziki , ila kuna tukio lilitokea ni Mwanamuziki wa kimataifa ambaye ni hayati kwa sasa James 'Cool James' mtoto wa Dandu alienda Bongo Records na mwanamuziki mkubwa sana Afrika na dunia si mwingine ni hayati Madilu System , kwa ajili ya kurekodi wimbo 'Mamou Remix' .
P Funk alipomwona Madilu na aina ya muziki anaoufanya akajua hapa kazi ipo , ila akaona sio shida yupo hapa Alain 'Cente' Mapigo mkali wa hizo kazi atamaliza shughuli , P akamkabidhi kazi hiyo Alain Mapigo na Alain bila tashwishwi akafanya 'unyama' wake na kuipika ngoma ya kimataifa 'Mamou Rmx' ya Cool James Ft Madilu System.
Nitakupa zazamani kupitia Chamber Media endelea kufuatilia.
Mwisho.
.jpeg)
Post a Comment