Na Ismail Luhamba
Wajumbe wa UWT kutoka katika Kata 28 Wilaya ya Ikungi wameahidi kuwa tarehe 29, Oktoba kura zote watampatia Rais Dokta Samia Suluhu Hassan hii kutokana na mazuri aliyoyafanya katika kipindi cha miaka minne ya utawala wake.
Hayo yamesema jana Oktoba 03,2025 ambapo wajumbe wa kata 28 za walaya ikungi mbele ya kamati ya Uratibu ya UWT kanda ya kati iliyo chini ya Mwenyekiti Dina Chilolo na wezake ,ambapo wanatembelea walaya zote za Mkoa wa Singida kusaka kura za wangombea wa Chama Cha Mapinduzi.
Wamesisitiza kuwa hawana chama mbadala zaidi ya CCM. Wamesema wanaona matunda ya awamu ya Sita kupitia maboresho ya miundombinu, barabara na mazingira ya biashara.
Kamati hiyo imewataka UWT kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia, akibainisha kwamba Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa kinamama,vijana na wafanyabiashara, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.




Post a Comment