SAJJAD: OKTOBA 29 KURA ZOTE KWA SAMIA, GULAMALI NA MADIWANI WOTE WA CCM

 

Na Thobias Mwanakatwe,ILONGERO 



KADA wa Chama Cha Mapinduzi ambaye alikuwa mtiania ubunge Jimbo la Singida Mjini, Sajjad Haidery, ameshiriki uzinduzi wa kampeni jimbo la Ilongero na kutoa wito kwa wananchi Oktoba 29, 2025 wawapigie kura za kutosha wagombea wa CCM ambao ni rais, wabunge na madiwani.



Amesema zipo sababu kuu ambazo zinawafanya wananchi wamchague mama Samia Suluhu Hassan na kukichagua Chama Cha Mapinduzi kwani katika kipindi kifupi cha miaka minne cha utawala wake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameleta maendeleo makubwa nchini hivyo akipewa miaka mitano ataweza kufanya makubwa zaidi.



Jimbo la Ilongero mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM ni Haiderali Gulamali.


MWISHO

Post a Comment

Previous Post Next Post