NYALANDU: TUNATAKA TUMHESHIMISHE SAMIA KWA KURA ZA KISHINDO ZA CCM

 

Thobias Mwanakatwe,ILONGERO



KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri mstaafu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu, amewataka wananchi kila mwenye kadi ya kupigia anaowajibu wa kuulinda Mkoa wa Singida kwa kumpigia kura ili kumheshimisha mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.Samia Suluhu Hassan,wagombea ubunge na udiwani.


Nyalandu akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Ilongero Haidery Gulamali uliofanyika kata ya Mtinko, amesema Mkoa wa Singida ambao ni wa CCM ni lazima uchaguzi wa mwaka huu uongoze katika kura za kishindo kwa wagombea wote wa CCM.



"Nitasimama pamoja na mgombea ubunge jimbo la Ilongero,Gulamali na kuhakikisha mama Samia Suluhu Hassan anapata kura zote za ndio, tunataka watu wote watoke kupiga kura naungana na timu ya taifa kwa kutembelea kila mkoa na ndio maana kuna basi pale tunatembea nalo kusaka kula za kishindo za CCM kwa kila mkoa," amesema Nyalandu.



Aidha, Nyalandu katika kuhakikisha madiwani hawakwami katika Kampeni alitoa shilingi milioni 15 kwa madiwani 21 wa kata na madiwani 9 wa viti maalum ili waweze kupiga kampeni vizuri na kufika kila kata,kijiji na kitongoji kusaka kura za CCM.

Post a Comment

Previous Post Next Post