GULAMALI AYAKATAA MAKUNDI CCM ILONGERO

 

Na Robert Onesmo



Mgombea wa ubunge jimbo la Ilongero Mkoani Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Gulamali Haiderali ,amesema makundi yaliyotengenezeka kipindi cha mchakato wa kupata wagombea hayana nafasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi 



Gulamali ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa kampeni za ubunge na udiwani katika jimbo la Ilongero,ambapo Gulamali amekiri kuwa bila shaka kuna makundi yalitengenezwa katika kipindi cha mchakato wa upatikanaji wa wagombea, hivyo baada ya chama kurudisha wagombea walioteuliwa kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama chama Mapinduzi ni vyema wakawa kitu kimoja kwa ajili ya kuwatumikia wananchi. 



"Chama Cha Mapinduzi tunaendelea kutawala kwa sababu ni wamoja na wenye mshikhamano hivyo lazima tuvunje makundi ili kukijenga zaidi chama hichi"amesema Gulamali. 



Kwa upande wa Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Martha Mlata amesema Chama kimerudisha wagombea makini akimtolea mfano Gulamali Haiderali kuwa kijana mtiifu wa chama chama Mapinduzi na  mwenye usikivu wa hali ya juu

Post a Comment

Previous Post Next Post