CHIFU MGONTO: WANASINGIDA MJINI MTUMENI YAGI KIARATU AENDE BUNGENI


Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA



MGOMBEA ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Ikungi Mashariki, Chifu Thomas Mgonto, ameshiriki uzinduzi wa kampeni katika jimbo la Singida mjini huku akiwaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua Yagi Kiaratu li aweze kwenda bunge.


 



Chifu Mgonto akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika soko kuu la Singida mjini, amesema mgombea ubunge jimbo la Singida mjini ni jembe  Yagi Kiaratu ni jembe kweli hivyo wakimchagua na kumtuma kwenda bungeni ataweza kuwawakilisha vyema na kuleta maendeleo makubwa katika jimbo hilo.



“Kamati Kuu ilipoketi Dodoma ikajiulize nimtume nani Singida mjini ,wakauliza Halmashauri Kuu ya CCM tumtume nani pale Singida mjini, baada ya kuuliza ikasema kuna yule anayejua mitaa yote ya Singida mjini, kuna yule anayejua barabara zote za Singida mjini, anayefahamu vizuri soko la Singida mjini, anayefahamu huduma za afya, anayefahamu shule zote naye ni Yagi Kiaratu,”……..



Katika kuthibitisha kwamba Kiaratu ni jembe, Chifu Mgonto alitoa ushuhuda…..“Kuna siku nilikuwa nimeketi na Yagi Kiaratu wakati tunapitia ilani ya CCM ukurasa baada ya ukurasa ndani ya dakika tano mimi nikiwa ukurasa wa 22 yeye yupo ukurasa wa 66, nadhani mnaona spidi yake ilivyo ya hali ya juu, huyu ni mama wa viwango, ni mama wa spidi ni mama anayechapa kazi kwa kuona tu ile ilani alivyoichakata ndani ya dakika tano,hakika singida mjini mumepata jembe kweli,” amesema Chifu Mgonto.

Post a Comment

Previous Post Next Post