Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri mstaafu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu atahakikisha anapiga kampeni nzito ambazo zitaufanya Mkoa wa Singida kuongoza Tanzania kwa kura nyingi za CCM.
Amesema hayo leo (Septemba 2, 2025) wakati akizungumza na mamia ya wananchi walioshiriki mkutano wa uzinduzi wa kampeni katika jimbo la Singida Mjini kwa ajili ya kumnadi mgombea urais kupitia CCM Dk.Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa jimbo hilo, Yagi Kiaratu na wagombea udiwani kutoka kata 18 za Manispaa ya Singida.
“Chama hiki kimetutoa mbali, chama hiki ni kikubwa kuliko mgombea mmoja mmoja, tunataka tarehe 29, Oktoba kura za CCM Singida ziongoze Tanzania,mikoa itashindana tunataka ahadi yetu ya kumpa mama Dk.Samia Suluhu Hassan ziongoze, tunataka kura za wabunge zikiongozwa na Yagi Kiaratu ziongoze,”amesema Nyalandu huku akishangiliwa na mamia ya wananchi walioshiriki mkutano huo.
“Kesho (Jumatano) tunakwenda Ilongero, tutakwenda na kwa Tundu Lissu tuhakikishe tunamsogeza mbele zaidi, tunataka tuhakikishe chama hiki ambacho kina historia kubwa na Mkoa wa Singida kinapata ushindi wa kishindo kwani Mwalimu Julius Nyerere aliagiwa hapa hapa Singida,”……..
Aidha, Nyalandu ameahidi kuwa wakati wa kampeni “Tutakuwa pamoja nyumba kwa nyumba, tawi kwa tawi, kata kwa kata,jimbo kwa jimbo na kama mnavyoona tunatembea na basi kubwa la Mama Samia tutakwenda pia mikoa yote,’ amesema.



Post a Comment