TAKUKURU SINGIDA YAPIGA KAZI YAOKOA PESA



Na Amini Nyaungo


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imeokoa shilingi milioni 35,017,556.10 kutokana na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo 23 katika sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu.

Katika ufuatiliani wa kutekeleza jukumu hilo TAKUKURU Mkoa wa Singida ulifuatilia matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ishirini na tatu yenye thamani ya shilingi 7,471,033,798.00.

Baada ya ufuatiliaji huo wamebaini kuwa kiasi cha shilingi 186,770 zilikatwa kwa kutoa huduma kama ushuru wa huduma katika miradi ya ujenzi wa shule ya Sekondari Mtoa Darajani bila kuwasilishwa kws Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Iramba.

Huku sh 20,848,585 zilikatwa kwa wazabuni kama kodi ya ya zuio katika miradi ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Amali Msange na Mtoa Darajani pamoja na kituo cha Afya Ngiju lakini hazikuwasilishwa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA.

Shilingi 13,340,680 zililipwa kwa wazabuni bila kuleta vifaa katika shule za sekondari Amali- Msange,Kijtoa, Kidarafa na Mto Darajani, Kintinku na Shule za Msingi Chidamsulu na Kijota.

Shilingi 641,520 zililipwa kwa mzabuni ikiwa ni kodi ha ongezeko la thamani(VAT) katika mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu (2 kwa 1) katika shule ya Sekondari Utemini huku Mzabuni huyo akiwa hana sifa za kulipwa VAT.

Baada ya kubaini mapungufu hayo ofisi ilichukua hatua zifuatazo, kurejeshwa kwa kiasi cha sh. 20,848,585 kwa Mamlaka ya mapato Tanzania kama kodi ya zuio, vifaa vyenye thamani ya shilingi 13,340,680 vimefikishwa katika shule ya sekodari Amali- Msange, Kijota, Kidarafa, Mtoa Darajani  Kintinku na shule ya Msingi Chidamsulu na Kinogo na kutumika kama ilivyokusudiwa.

Kuwasilishwa kwa kiasi cha shiling 186,770 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kama Ushuru wa huduma  pamoja na Kurejeshwa kwa kiasi cha Shilingi 641,520 kwenye akaunti ya shule ya Sekondari Utemini.

Aidha TAKUKURU Mkoa wa Singida wamefanya elimu kwa Umma na kuwafikia Wananchi  6632 kupitia semina 42, Mikutamo  ya hadhara 15 maoneyesho matatu vipindi vya Radio vitatu na utoaji wa habari mbili za uimarishaji wa klabu 40 katika shule za Msingi, Sekondari pamoja na vyuo.

Kwa elimu ambayo imetolewa imesaidia wananchi kuhamasika kushiriki katika mapambano  dhidi ya rushwa.

Pia katika kampeni ya TAKUKURU rafiki katika utekelezaji wake uliendelea kwa kufanya vikao mbalimbali katika kata 21 ambapo kero 88 ziliibuliwa na kutatuliwa.

Malalamiko 75 yalipolelewa ambapo 51 yalihusu vitendo vya rushwa na 24 hayakuhusu vitendo vya rushwa ambapo wahusika walishauriwa.

Aidha mashauri 23 yaliendeshwa mahakamani ambapo nane ni mapya, mahsauri manne yalitolewa uamuzi na Jamhuri kusjinda matatu.

Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post