Na Amini Nyaungo
Wananchi wameaswa kutumia nishati safi ya kupikia ili kuendelea kutunza mazingira na kuokoa afya za watumiaji ambao wanatumia nishati zinazoharibu mfumo wa afya zao zikiwemo Mkaa.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida Ibrahim Solo, amesema kuwa leo wametoa elimu kwa wananchi katika kutumia nishati safi ya kupikia ambapo elimu hiyo wameitoa katika banda lao lililopo viwanja vya Bombadia katika mkesha wa Mwenge huku akiahidi kuwa wataendelea kutoa elimu hiyo sehemu mbalimbali.
"Leo tupo hapa katika huu mkesha wa Mwenge na tutaendelea kutoa elimu hii ya nishati safi ya kupikia ili wananchi wapate kuelewa na kutumia, tunavyo vifaa ambavyo tutawaonesha kabisa namna ya matumizi yake"Solo
Aidha amebainisha kuwa vifaa ambavyo wamevileta ni mfano wa kuonesha namna gani nishati safi inatumika kwa kupitia umeme.
"Tumekuja na vifaa hivi lengo waone vile inavyotumika na wawe tayari kwa ajili ya matumizi yake," Ameongeza
Wakati huo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru 2025 Ismail Ally Ussi ameweka wazi kuwa kutumia nishati safi ya kupikia ni kuunga mkono juhudi za Daktari Samia Suluhu Hassan katika kuwanusuru wanachi wake katika maswala ya Afya.
"Ni jambo zuri kutumia nishati safi ya kupikia kwani haiathiri afya lakini kufanya hivi ni kuunga mkono jitihada anazozifanya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan katika kampeni yake kwa nchi za Afrika.
Kwa upande wa Agnes Proser kutoka kampuni ya Jicho Chanya ambapo alitumia banda la TANESCO Mkoa wa Singida kutoa elimu juu ya vifaa walivyovileta amesema kuwa matumizi ya nishati safi ni rahisi na gharama yake nafuu maana inatumika Uniti moja ya kupikia kwa saa moja halichafui mazingira.
"Matumizi yake ni mazuri mno na rahisi unatumia Unit moja kwa saa ukitumia haya majiko ya umeme," Agnes.
Shirika la umeme Tanesco Mkao wa Singida leo watakesha katika Mkesha huo wa Mwenge wa Uhuru na wanaendelea kuwakaribisha wote wanaotaka kujua matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Mwisho



Post a Comment