CCM KUUKARABATI UWANJA WA LITI SINGIDA

 NaJumbe Ismailly SINGIDA



WAMILIKI wa uwanja wa mchezo wa mpira wa miguu wa kumbu kumbu ya LITI uliopo Mjini Singida, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida wameanza kukarabati miundombinu yake ya uchumi ikiwemo, uwanja wa mchezo wa mpira wa miguu wa Liti na ukarabati huo utafanyika kwa awamu,
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Elfasi Lwanji amesema ukarabati huo ulioanza kwenye jengo la chama, na mara utakapokamilika,ndipo ukarabati wa miundombinu ya uwanja wa michezo utakapoanza, ikiwani pamoja na kuweka taa, kuweka majukwa ya kukaa mashabiki ili waweze kushuhudia shughuli zozote zinazofanyika katika uwanja huo.
Katika hatua nyingine Chama Cha mpira wa miguu wilaya ya Singida (SIDIFA) kimesema kinatarajia kusimamia mashindano ya kugombea kombe la DSAM CUP inayotarajia kuanza wakati wowote  wiki ijayo katika viwanja vya michezo vya shule ya msingi Ukombozi, Manispaa ya Singida na kutangaza zawadi zitakazotolewa kwa washiriki wa ligi hiyo.
Kwa upande wa ligi ya watoto wenye umri chini ya miaka 13 pamoja na ligi ya watoto wenye umri chini ya miaka 11, inatarajia pia kuanza kutimua vumbi mwezi wa tisa mwaka huu.
MWISHO.

Post a Comment

Previous Post Next Post