Na Amini Nyaungo
Shirika la Sense International kupitia mradi wao wa kuwazesha vijana wenye mahitaji maalumu kupata mafunzo wametoa vifaa vya kisasa vya kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili viwasaidie katika elimu chuo hapo.
Hayo yamefanyika jana na Afisa Mradi wa Sense International Emiliana Protas Rutakyamirwa ambapo amesema kuwa vifaa hivyo wamevitoa wakiwa na wafadhili wao ambao ni Faroe Island na Hodge Foundation.
Aidha Emiliana amsema kuwa vifaa hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi hao na chuo kwa ujumla ili wapate mafunzo bora na ustawi.
" Vifaa hivi ni kwa ajili ya wanafunzi kuwawezesha wanafunzi ili kuwawezesha kuongeza ufanisi wao wa kumudu mazingira na wanapokuwa darasani,"Emiliana
Katika hatua nyingi wametoa vifaa kama vile Printer, Projekta, Compture, Viti na vifaa vya kufundishia wametoa vifaa kwa waliku Compture pamoja na Projekta.
Kwa Upande wa Mkuu wa Chuo hicho Fatma Malenga amesema kuwa vifaa higyo vitawasaidia kuwajengea uwezo wanafunzi ili wawe bora katika masomo yao.
Amesema kuwa vifaa ambavyo wamevipokea vitawasaidia katika ufundishaji bora kwa Sense International wamewapa Compture na vifsa bora vya kufundishia.
"Vifaa hivi kwa ajili ya wanafunzi ili kuwawezesha kuongeza ufanisi wa kumudu mazingira na darasani , kuna vifaa kwa ajili ya wanafunzi wenyewe darasani na vingine vya kufundishia,"Malengo.
Ametumia nafasi hiyo pia kusema kuwa wamezindua dawati la kijinsia chuo hapo ili wapate wigo moana pindi inapotoke maswala ya ukatili.
Mgeni Rasmi wa tukio hilo ambaye ni Afisa Ustawi Mkuu wa Mkoa wa Singida Edward amevigawa vifaa hivyo na kuweka bayana kuwa walicho kifanya Sense International ni alama nzuri na vitasaidia wanafunzi.
"Vifaa hivi kama vile viti mwendo, vifaa vya kusikia,fimbo nyeupe na projecta vifaa hivi vitawezehsa kushiriki vyema katika jamii,"Edward.
Mwisho.




Post a Comment