Na Amini Nyaungo
CHAMA CHA MAPINDUZI CCM
KIMEANZISHWA 05,02,1977 ikiunganisha vyama viwili vya siasa TANU NA Afro-Shirazi
Party (ASP) .
Viongozi wa vyama hivyo
baada ya kuona umuhimu wa Demokrasia ndipo mfumo wa vyama vingi uliundwa mwaka
1992 na uchaguzi wake Mkuu umefanyika mwaka 1995.
Tangu kupata Uhuru na
tangu Muungano wa Tanzania na Zanzibar hadi sasa CHAMA CHA MAPINDUZI ndicho
kinaongoza dola.
Na desturi ya vyama vya
siasa lazima kuwe na muongozo kwa kila baada ya miaka mitano ya uchaguzi mkuu.
ILANI ya CCM ya mwaka 2025
hadi 2030 ina vipaumbele vingi endapo watapata tenda ridhaa ya kuongoza nchi
ikiwa uchaguzi mkuu unatarajiwa ulifanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Chamber Talk Show
inakuletea vipaumbele 14 vya Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030 kama amabvyo
wamevieleza kupitia mkutano Mkuu uliofanyika mwezi Mae, 2025.
1. ARENA
Soko la ajira kwa vijana
walio wengi hivi sasa wapo katika Sanaa mbalimbali ikiwemo burudani ya muziki
hapa inajumuisha muziki wote iwe singeli, dance au bongo flava. Kupitia ilani
ya Chama Cha Mapinduzi inasema kuwa kama watapata ridhaa watatengeneza ukumbi
mkubwa wa burudani maarufu kama ARENA.
Rwanda ni sehemu nzuri ya
mfano na wasanii wa hapa nyumbani wamekuwa wakililia juu ya hili msanii kama Ali Kiba
Diamond wote wamekuwa wakihitaji jambo hili lifanyike.
Faida moja wapo ni mapato
katika matumizi sahihi ya Ukumbi huo wa burudani mapato ya ndani na nje ya nchi
maana lazima itatumika katika matukio mbalimbali.
2. MAJI 90%
Ilani yao ya uchaguzi pia
wamesema wata hakikisha kuwa asilimia 90 ya kaya zote zinafikiwa na huduma ya
maji safi na salama. Kila mmoja anajua umuhimu wa kuwa na maji ya uhakika CCM
wameiona hii na wamesema watahakikisha maji yanakuwa ya kutosha.
3. KUPUNGUZA BEI YA VIFAA
UJENZI
Katika kuhakikisha kuwa
wanaohitaji kujenga makazi yao hususani nyumba na sehemu ya biashara CCM
wanasema watapunguza bei ya bidhaa vya ujenzi.
4. KUKAMILISHA MRADI WA MAJI
Wamesema kuwa
watakamilisha miradi mikubwa ya maji katika miji 28 ili wananchi wake wanufaike
na upatikanaji wa maji muda wote.
5. UJENZI WA BANDARI MPYA
BAGAMOYO
Ili mapato yapatikane
lazima kuwepo na bandari salama za kupakua mizigo bahati nzuri Tanzania
tumejaliwa bahari hivyo moja ya mipango yao ni kujenga Bandari mpya ya
Bagamoyo Mkoani Pwani.
6. UMALIZIAJI WA SGR
Tayari SGR imetufikia
ikiwa kutoka DAR ES SALAAM hadi DODOMA sasa
ilani yao inasema kuwa watamalizia ujenzi wa SGR Kutoka DODOMA hadi
MWANZA, pia kumalizaia ujenzi kutoka DODOMA , TABORA HADI KIGOMA.
7. UJENZI WA OFISI NA NYUMBA
ZA WALIMU
CCM wamesema kuwa
watahakikisha watajenga nyumba za walimu pamoja na ofisi zaa walimu nchi nzima
ili walimu wawe katika wakati mzuri.
8. UNUNUZI WA NDEGE 8
Kuimarisha usafiri wa
anga ilani ya CCM inasema wataongeza ndege nane mpya kwa ajili ya shirika la
ndege ATCL.
9. AJIRA
Moja ya sehemu ambayo
inashida ni ajira kwa vijana sasa CCM wameona lazima jambo hili liwepo ndipo
wakasema watahakikisha watatoa ajira milioni 8.5.
10. KILIMO
Katika kilimo ambapo ndio
sehemu sahihi na ajira nyingi zinatoka shambani wamesema kuwa eneo lla kilimo wataongeza
eneo la kilimo cha umwagiliaji kufikia ekari milioni 5.
11. UMEME
Maendeleo ya nchi pia
lazima kuwe na mwanga hapa sasa wametuambia kuwa watafanya usambazaji wa umeme
kwa vitongoji vyote nchi nzimaa ambapo
kwa sasa kila kijiji kina umeme kilichobaki wamalizie ili wapate umeme katika
vitongoji vyote.
12. MATREKTA
Uanzishwaji wa vituo vya
Matreka na zana za kilimo kila kata hii ni moja ya mipango yao kuelekea
2025-20230.
13. BARABARA
Ujenzi wa barabara nne
kutoka IGAWA- UYOLE, TUNDUMA yenye kilomita 218 pamoja na barabara ya Kibaoni ,
Majimoto- Inyonga KM 162 kuendelea na ujenzi wa Baravbara ya Geita-
Bukoli-Kahama KM 133 lakini pia barabara ya Tarime- Mugumu km 87 pamoja na
Barabara ya Mabokeni- Maramba-Bombo-Mtoni- umba hadi Same km 278.
14. MIKOPO
Ili kuhakikisha wananchi
wake wanafanikiwa watahakikisha wanatoa mikopo kwa kampuni change na kazi za
ubunifu.
Hii ndio ILANI YA CHAMA
CHA MAPINDUZI (CCM) ikilenga kuimarisha watu wake wanao waongoza endapo
watapata ridhaa.
Mwisho















Post a Comment