Na Mwandishi Wetu
Chief Thomas Mgonto amechukua 'Form' kuwania ubunge jimbo la Ikungi Mashariki leo Juni 30,2025 katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Zoezi la kuchukua "Form'' limeanza tarehe 28 Juni na litatamatika July 2.
Kama atapata ridhaa kupitia CCM ya kuwakilisha Jimbo hilo Chief Thomas Mgonto atapeperusha bendera hiyo.
Mgonto ni mzaliwa wa Ikungi maeneo ya Siuyu ni msomi na mfanyabiashara ambapo maarufu zaidi katika Wilaya hiyo kwa kombe lake la vijana katika mpira wa miguu yaani "Mgonto Cup" ambapo mwaka huu limefanyika Siuyu.
Mwisho
Post a Comment