KIKWETE NA WCF WAGUSWA: WATATUA CHANGAMOTO ZA WATU WENYE ULEMAVU


Na Amini Nyaungo



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu kazi ajira na watu wenye ulemavu  Ridhiwani Kikwete, leo amekabidhi vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu katika chuo cha ufundi na marekebisho Saba saba mkoani Singida.



Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na viti mwendo, fimbo pamoja na karatasi maalumu za kuandikia kwa watu wenye ulemavu wa macho ambavyo vimetolewa na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF)kama sehemu ya kuadhimisha miaka 10 toka kuanzishwa kwa mfuko huo.



Akizungumza katika tukio hilo waziri Kikwete ameupongeza mfuko wa WCF kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha kundi la watu wenye ulemavu wanakuwa na vifaa saidizi.



"WCF mnafanyakazi kubwa sana katika kuwaunganisha jamii hii sio hapa tu Singida bali nchi nzima,"Kikwete



Kikwete hakuacha kumsemea mazuri Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya huku akiweka wazi kuwa WCF kazi wanayoifanya ni maelekezo ya Rais Samia.



Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Bi Halima Ndegengo amepongeza WCF kwa kuwatahimi walengwa katika chuo Saba saba.



"WCF wangeweza kupeleka sehemu nyingine yoyote lakini wameona wapeleke Singida ahsanteni sana,"Dendego

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dr John Mduma, ameelezea jinsi wanavyoguswa na makundi mbalimbali

"Tunaguswa na mambo haya ili kuweka jamii karibu na pamoja na tutaendelea kufanya zaidi," DR Mduma



 Kwa upande wa Mkuu wa Chuo hicho Fatma Malenga amebainisha chuo kinavyoendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wanafunzi walemavu.



Kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita WCF imetumia zaidi ya shilingi bilioni moja katika kurejesha kwa jamii.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post