Na Amini Nyaungo, Singida
Wananchi wameaswa kushirikiana
kwa karibu na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wote na hata yanapotokea
majanga ya moto au maokozi ili jeshi hilo liweze kutoa msaada wake kama ilivyo
adhima na lengo la Jeshi la Zimamoto.
Hayo yamefanyika leo (Mei
3,2025) na Jeshi la Zimamoto Mkoani
Singida walipokuwa wanashiriki zoezi la kufanya usafi katika makaburi
yaliyopo kona ya Mohamedi mkoani Singida
ikiwa katika kuadhimisha wiki ya Zimamoto ambao katika makaburi hayo wahanga waliunguaa
na moto kutokana na ajali ya gari mwaka 2007.
Akiongea na Chamber Media
mara baada ya kufanya usafi katika eneo hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji Mkoa wa Singida Mrakibu Devotha Bigawa amesema kuwa wametumia wiki
ya Zimamoto Mkoani Singida kushiriki katika shughuli za kijamii hususani
kuwakumbuka waliowahi kupata ajali ya gari mwaka 2007 kona ya Mohamed ambao
walikuwa 26.
“ Siku ya leo tumekuja
kuwaenzi wenzetu waliotangulia mbele ya haki tupo maeneo haya kwa ajili ya
kufanya usafi, tupo katika wiki ya Zimamoto ambayo imeanza April 28 na
kuhitimisha Mei 4 mwaka huu, tumeamua kufika siku hii ya leo Jumamosi,”
Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi waweze kushrikiana kwa karibu na
Jeshi la Zimamoto pindi wanapopata majanga ya moto ili waweze kusaidia kuokoa
kama ambavyo ilivyo azma ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
“Niwaase wenzangu pale
unapoona kadhia yoyote inatokea piga 114 ili msaada wa haraka upatikane, hivyo
tushirikiane,” Bigawa
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa Mtaa wa Kimpungua Jumanne Shabani Mahame amewashukuru Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji kwa kufika na kuwakumbuka ndugu zao waliotanguia mbele ya haki kwa ajai
hiyo.
“Kwa sasa tunayo namba
104 hivyo tukiona ajali tutapiga ili watusaidie tunawashukuru sana kwa ujio
wenu hapa,” Jumanne
Aidha amesema kuwa ajali
hiyo ilitokea tarehe 15,06,2007 eneo la kona ya Mohamed na watu 26 walipoteza
maisha na kuungua moto hivyo kufanya wote kuzikwa eneo hilo.
Katika zaoezi hilo Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji waliambatana na Mabalozi wa Usalama Barabarani
akiwakilishwa na Khadija Omary amesema kuwa wako tayari kutumika wakati wowote
hivyo wamejisikia furaha kuungana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
“Tumefurahi kuungana na
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji sisi tupo tayari wakituhitaji tutafika kuungana
nao na sisi tukiwahitaji tutawaomba ili tushirikiane,” Khadija.
Kwa upande wa wananchi wa eneo hilo Jeni Shabani amesema
hivi sasa wanaukaribu na watu wa usalama sio kama zamani hivyo kufika kwa jeshi
la Zimamoto na Uokoaji ni sawa na kuzidisha ushirikiano
Mwisho
Post a Comment