Na Amini Nyaungo
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan amepongezwa na mtoto wa aliyekuwa
Rais wa awamu ya tano Dokta John Pombe Magufuli ambaye ni Jesca Magufuli
alipokuwa anaongea katika mahojiano na Millard Ayo.
Jesca amesema kuwa tangu
kufariki kwa Dokta Magufuli Rais Dokta Samia Suluhu Hassan hakuwahi kuacha kuja
kuwaona pamoja na kuwasomesha baadhi ya watoto ambao wanasoma chuo kwa kulipa
ada.
Kupitia mahojiano hayo Millard
Ayo amemuuliza Jesca kuwa Rais Dokta Samia amekuwa mtu wa faraja namba moja kwa
Taifa je katika familia hiyo ilikuwaje ?
Jesca amesema kuwa “Mama
amekuwa nasi tangia mwanzo nakumbuka hata kipindi mzee alipofariki baada ya
kuapishwa alikuja nyumbani siku hiyo hiyo akamuahidi mama kuwa sitokuacha kama
kuna changamoto zimetokea usisite kuniambia mdogo wangu, kuanzia matibabu ya bibi yetu mama
Samia aliendelea wale manesi hadi leo wapo wanaendelea kumuhudumia bibi,
kipindi mzee anafariki sisi wengine tulikuwa tumeajiriwa kuna wadogo zetu
walikuwa wanaasoma hadi sasa wanalipiwa ada ya chuo, na mengine mengi sio hayo
tu siwezi kuyataja yote ila hayo ni machache,” Jesca
Jesca ameongeza kuwa Rais
Samia ameweza kuendesha nchi vizuri kwani miradi mbalimbali ya maendeleo anaendelea
kuimalizia ikiwemo Daraja la Kigongo Busisi.
Kwa upande wa timu gani
anaipenda Jesca hajaweka wazi akisema kuwa hayati Dokta Magufuli alikuwa
anapenda sana mifugo ila mpira sio sana huku miziki ndio alikuwa anasikiliza
ikiwemo miziki ya zamani na ya sasa.
Jesca amesema msanii
ambaye alikuwa anamsikiliza zaidi ni TIMBULO alikuwa namsikiliza sana.
“Kwenye mpira hapana ila
miziki alikuwa anamsikiliza sana Timbulo, alikuwa anasikiliza nyimbo zake mno.
Jesca amesema msiba wa
baba yake taarifa alipata kupitia mitandao kama wengine huku akihadithia maisha
yake ya chuo hayajabadilika licha ya kuwa baba yake alikuwa Rais.
Mwisho



Post a Comment