HANJE AAMUA KUZAMA CCM

Na Amini Nyaungo



Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa kundi la vijana Nusrat Hanje ambaye alikuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) atahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kuunga mkono jitihada anazofanya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kuanzia sasa hadi mwezi wa saba atahamia CCM.

HANJE ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara kwa wananchi waliokusanyika katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida

Aidha katika moja ya maneno yake amesema kuwa amegundua kuwa watu wanataka kutatuliwa shida zao hii inatokana na uzoefu alioupata katika kipindi cha miaka mitano aliyokaa BUNGENI.

Katika hatua nyingine amesema kuwa Rais Dokta Samia anafanyakazi nzuri halali usiku na mchana hivyo ni vyema akahamia CCM muda mchache ujao kutokea sasa hadi mwezi was aba.

“katika Tanzania na Mkoa wa Singida mama anapambana kinomanoma, mama anapambana anapiga kazi usiku na mchana, nimeamua mwenyewe bila ya kulazimishwa mwenyewe kwamba muda wowote kutokea hivi sasa hadi mwezi was aba nitahamia CCM,”Hanje

Katika Mkutano huo pia Hanje amewataka wanaikungi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono kuhamia CCM kwa kuwa tayari changamoto zao na kero zao zinaweza kutatuliwa bila kusababisha vurugu wala machafuko.

Mwisho 

Post a Comment

Previous Post Next Post