Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, katika uchaguzi uliofanyika leo Mei 18, 2025, Geneva-Uswisi
Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile, aliyefariki dunia Novemba 2024
Wagombea wengine waliowania nafasi hiyo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na Prof. Moustafa Mijiyawa kutoka Togo, Dkt. N’Da Konan Michel Yao kutoka Ivory Coast, Dkt. Boureima Hama Sambo wa Niger na Mohamed Lamine Dramé kutoka Guinea
Aidha, Kwa mujibu wa utaratibu wa WHO, Prof. Janabi anatarajiwa kuhudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha Miaka Mitano, huku akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine mmoja pekee



Post a Comment