MWAMBAPA : VIJANA UKIONA MWENZAKO AMEPEWA NAFASI USIMTENGENEZEE AJALI

 

Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA 



MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya, Medson Mwambapa, amewataka vijana kupendana na kushirikiana ili kuijenga jumuiya iliyo imara na kwamba hakuna sababu mwenzako anapopewa nafasi (cheo) unamtengenezea ajali.


Amesema hayo leo (April 9, 2025) wakati akizungumza na viongozi wa UVCCM wa wilaya zote za Mkoa wa Singida baada ya kupita kuwasalimia wakiwa kwenye kikao ambacho kilikuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida,Zulfat Muja.


"Mfumo wa nafasi tulizoaminiwa vijana ni vizuri kupendana ukiona mwenzio amepewa nafasi usimtengenezee ajali, yapp makundi kwenye vijana ambayo kazi yake kubwa ni kutengeneza fitina,tuyaepuke tusapoteane kwenye kazi kwasababu alipo mwingine unaweza kupanda wewe," amesema Mwambapa.



Mwambapa amesema vijana lazima watambue kuwa maisha ya siasa hayana adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu.


"Leo kuna katibu wa hamasa kuna siku moja atatamani awe Mwenyekiti apande hadi ngazi ya mkoa kwa hiyo vijana tukipendana ni rahisi sana kufanikiwa," amesma Mwambapa.


Mwambapa amesema sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inawajenga vijana kuwa na umoja na ushirikiano.


Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post