Na Robert Onesmo
Jana wakati Barcelona wanawaangamiza Borussia Dortmond pale Comp Nou katika michuano ya UCL, ilipofika dakika ya 81 kinda Lamine Yamal alionyesha ishara ya kutaka kutolewa lakini ilichukua muda kidogo mpaka kutoka kilichoshangaza wengi nyota huyo hakuwa anahisi maumivu yeyote jambo ambalo limefanya waandishi wa habari wamuulize ,..hapa alinukuliwa akisema
"Nilihisi maumivu kidogo nikawa namuomba kocha anibadilishe huku nikiomba amuingize Ansu Fati ,yeye ni mwenzetu tunapaswa kumsaidia na tunatamani arejee kwenye ubora wake" alisema Lamine Yamal.
RAPHINHA ,LEWANDOWSK WAVUNJA REKODI YA MESSI NA NEYMAR UCL BAADA YA MIAKA 10
Nyota wa Barcelona Rafael Dias Bellol maarufu kama Raphinha pamoja na Robert Lewandowsk , ambao kwa sasa wanafanya vyema katika michuano mbalimbali ikiwemo ya Uefa Champions league, wamevunja rekodi ya nyota wawili wa zamani wa timu hiyo (Neymar&Messi)ambayo waliiweka miaka 10 iliyopita katika michuano ya UCL.
Hizi ni takwimu zao za magoli.
UCL 2014/15:
🇦🇷Leo Messi: 10 Goals
🇧🇷Neymar: 10 Goals
UCL 2024/25:
🇧🇷Raphinha: 12 Goals
🇵🇱Lewandowski: 11 Goals
NB:RAFA NA ROBERT BADO WANAGAME ZINGINE MSIMU HUU WENDA WAKAWEKA REKODI NGUMU SANA KWA VIJANA WANAOKUJA KATIKA TIMU HIYO.
Mwisho



Post a Comment