Na Boniphace Jilili,Singida
Watumishi wapya wa umma walioingia kazini hivi karibuni wametakiwa kufanya kazi kwa weledi kulingana na nafasi zao kwa ajili ya ustawi wa Taifa.Hayo yamezungunzwa jana (Marchi 18,2025) na Mstahiki Meya Yagi Maulid Kiaratu katika semina elekezi kwa watumishi wa ajira mpya Manispaa ya Singida ambapo Meya amewaasa walioingia kazini kufanyakazi kulingana na mipaka na kazi zao.
Hata hivyo Mheshimiwa Yagi Kiaratu anawakumbusha suala la maadili katika utumishi wao kwani hiyo ndio silaha ya kuwafanya wao kuendelea na utumishi huku wakijenga mahusiano mazuri na jamii pamoja na viongozi wengine.
"Mnatakiwa kuwa na maadili kazini hiyo ndio silaha yenu ya kufanyakazi kwa muda mrefu na kupata maelewano," YagiMwisho
Post a Comment