Na Charles Kikoricho
Jumla ya minara 32 yenye thamani ya bilioni sita nukta nne.(6.4)ya watoa huduma wa mitandao ya mawasiliano imewashwa katika Mkoa wa Singida.Taarifa hiyo imetolewa Machi 16/2025 na Mtendaji Mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote Mhandisi Peter Mwasalyanda mbele ya kamati ya kudumu ya hesabu za serikali (PAC) chini ya kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo Joseph Kakunda katika kijiji cha Mbelekese wilaya ya Iramba Mkoani Singida ilipokuwa ikikagua mnara huo.
Mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote Mhandisi Peter Mwasalyanda amesema kuwa minara 14 inafadhiliwa na Benki ya dunia kupitia mradi wa Digital Tanzania na minara 18 inagharamiwa na mfuko wa mawasiliano kwa wote na mpaka sasa kwa mkoa wa Singida minara 14 imeshawashwa na inaendelea kutoa huduma ikiwa ni pamoja na ambao umetembelewa na kamati hiyo na minara mingine 18 inaendelea na ujenzi ikiwa katika hatua mbalimbali. Akitoa ufafanuzi wa mnara huo Mhandisi Peter Mwasalyanda Mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge hesabu za serikali (PAC) amesema kuwa mnara huo umejengwa na kampuni YAS Tanzania ,mfuko wa mawasiliano kwa wote umetoa ruzuku ya milioni mia moja ishirini na tano laki mbili na elfu 35 na mnara huo ulikamilika mwezi wa nne mwaka jana 2024 na kutoa huduma za 2G, 3G na 4G .
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ya Mbelekese Omary Shabani amesema kuwa kupatikana kwa mnara huo imekuwa fursa kwao kupata huduma nzuri za mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na ndugu na marafiki.Wananchi wa kata hiyo wamesema kuwepo kwa mnara huo kumerahisisha huduma za mawasiliano kwenye eneo lao na watatumia mawasiliano hayo kwaajili ya shughuli za maendeleo kama vile kujua bei za mazao na kutangaza biashara zao mtandaoni na kupata taarifa ya matukio mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya nchi.
Mikataba ya Ujenzi wa minara 758 nchi nzima ilisainiwa Mei 13, 2023 Dodoma na ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo Mkataba huo ni wa utekelezaji wa miaka miwili na mradi ulikuwa na maeneo mawili ya utekelezaji eneo la kwanza ilikuwa ni kujenga minara mipya 758 na eneo la pili ilikuwa ni kupandishwa hadhi kwa minara iliyokuwepo ili kutoka kwenye 2G na kwenda kwenye 3G, 4G na kuendelea na mradi huu unathamani jumla ya bilioni 126 ambapo fedha hizo zimegawanyika kutoka sehemu mbili kutoka mfuko wa mawasiliano kwa wote bilioni 70 nukta tatu (70.3) na kiasi cha bilioni 55 .7 kutoka Benki ya Dunia kwenye mradi ambao unaitwa Digital Tanzania mpaka sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia hamsini na sita.
Post a Comment