WANAWAKE WAONDOE MAWAZO MGANDO WANAWEZA- DENDEGO

 

Na Amini Nyaungo
Wanawake Mkoa wa Singida wametakiwa wajitambue na kuamua kugeuza mawazo yao pamoja na kuondoa mawazo mgando ya kutojiamini kuwa hawawezi kufanya mambo makubwa wanatakiwa wachukue mfano wa wanawake ambao walioweza ili wajitambue na kujua kuwa wanawaza kuwa chachu ya maendeleo.

Hayo ameyasema jana(February 7,2025) Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa yamefanyika katika uwanja wa Bombadia.

" Mwanamke wewe hakuna jambo litakalokushinda kama utaamua kupitia maadhimisho haya kuondoa mawazo mgando na kusema mwanamke anaweza,"Dendego.

Aidha katika hatua nyingine amewapongeza watu wa Wizara ya nishati kuwa kuwapa majiko ya gesi elf ishirini na tisa kwa ajili ya kaya mbalimbali mkoani Singida.

Katika amelezo yake amesema kuwa majiko hayo ni maelekezo ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan huku majiko hayo ameyaleta kwa gharama ya shilingi elf ishirini na mia nane ili kuwapunguzia gharama zaidi.

Ametumia fursa hiyo kuwaomba wajasiliamali wanawake kuwekeza katika ujazaji wa mitungi ya Gesi.

"Nitumie fursa hii kuwaambia wanawake mtumie nafasi hiyo unaweza kutumia mikopo ya Halmashauri kuwa mawakala wa gesi," Dendego.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata amesema kuwa Mkoa wa Singida umekuwa na ushirikishwaji wa kufursa katika kuleta maendeleo kwa viongozi wengi waliopo ni wanawake.

Ameweka wazi kuwa mkoa huo unaongozwa na wanawake na maendeleo yanakuja kwa kasi kwa ustadi wanaoufanya, pia hakuacha kuwashukuru wanaume katika ngazi mbalimbali.

Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post