MEI MOSI KUFANYIKA SINGIDA 2025

 Na Amini Nyaungo

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani mwaka huu kitaifa itaadhimishwa Mkoa wa Singida ambayo itafanyika (Tarehe mosi Mei 2025).

Hayo amesema Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego hapo jana baada ya kuwakaribisha katika Futari viongozi mbalimbali wa dini na Serikali iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa.

Dendego amesema kuwa ni bahati msimu huu kuweza kuyapokea maadhimisho ya siku ya wafanyakazi na ugeni mkubwa utakuja mkoani hapa.
"Singida tunayo bahati kubwa mwaka huu tutaadhimisha siku ya wafanyakazi mkoani kwetu na tunategemea ugeni mkubwa," Dendego.

Aidha katika maelezo yake Dendego amesema kuwa watu waendelee kutunza amani na utulivu ili mambo ya maendeleo yaendelee kufanyika kwani kukiwa hakuna amani hakuna kitakachofanyika.

Pia ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha watu wote kuhudhuria maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo maadhimisho kimkoa yatafanyika uwanja wa Bombadia siku ya leo ya (Tarehe 7,03,2025) huku maadhimisho kitaifa yatafanyika kesho (Tarehe 08,03,2025) mkoani Arusha.
Katika hatua nyingine Sheikh Mkuu wa Singida Issa Nasoro  amewaambia viongozi wa Serikali kutoiba mali za umaa kwani Mungu hapendi.

Amesema kuwa majibu ya ukame yanayotokea hivi sasa ni kwa sababu ya maovu ambayo yanaendelea kutendeka hivyo watu wote na dini zote warudi kwa matendo mema ili wapate baraka za mwenyenyezi Mungu.

" Ukame huu tulionao ni dhulma  na madhambi yetu hivyo turudini katika njia iliyonyooka," Dendego.

Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post