Na Amini Nyaungo
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Martha Gwau amewataka Umoja wa Wanawake Wilaya ya Ikungi (UWT)
kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Serikali
inayoongozwa na Rais Daktari Samia Suluhu Hassan ili waweze kujikomboa kiuchumi
na familia zao.Semina hiyo
ameigharamia na kuhusisha kada mbalimbali za wataalam wakiwemo Maafisa
Maendeleo, Watu wa Benki, Watu wanaohusika na mbolea pamoja na watu wa Mbegu
akiwa na lengo la kuwapa elimu kina mama katika Nyanja mbalimbali za maendelo.
Katika hatua nyingine Gwau amempongeza Rais Dokta Samia
Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika jamii ya Kitanzania.
“Rais Samia anaendelea kutuonyesha namna gani anaupendo kwa
wananchi hasa katika kuleta fursa na miradi ya maendeleo naomba tuendelee
kumuunga mkono,” GwauKatika semina hiyo alihudhuria Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Tano Likapakapa amempongeza Mbunge huyo
kwa kazi nzuri anayoifanya.
Mwisho..



Post a Comment