VIONGOZI WASAIDIENI KINA MAMA WAPATE MIKOPO- DENDEGO

 Na Amini Nyaungo

Maafisa Maendeleo ya jamii mkoani Singida wametakiwa wawasaidie kina mama ili wapate mikopo unayotolewa na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan ya asilimia kumi ambayo haina riba.

Hayo ameyasema jana (March 04,2025) Mkuu wa Mkoa wa Singi Dendego katika Ukumbi wa Chuo cha Uhasibu Singida katika hafla iliyondaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Martha Gwau.
Dendego amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii na viongozi wengine wawasaidie kina mama kupata mikopo huku akisisitiza masharti yasiwe magumu ambayo yatamfanya anayetaka mkopo ashindwe kukopa.
"Mumsadie mama apate mikopo , msiweke masharti magumu ambayo hawezi kuyatimiza, hakuna mama anayeahindwa kufanya biashara," Dendego

Katika hatua nyingine amewataka wafike leo katoka kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake ambapo leo ndio shughuli ya kimkoa inaanza hadi tarehe 7,03,2025.

Naye Mbunge wa Viti Maalum Martha Gwau amewalipia bima ya afya wanawake waliofika katika hafla hiyo ili wapate unafuu katika maisha yao.


Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post