Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja Andrew tarehe 3 Machi, 2025 amekabidhi Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora baada ya kuikarabati kwa Shilingi 14,700,00 (Milioni 14.7)
Mbunge Kainja amesema kuwa, ametimiza ahadi yake aliyoitoa mwaka 2023 wakati wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) lililofanyika Wilaya ya Urambo huku akikishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kumpa ushirikiano na kupokea mchango wake wa kujenga Chama Cha Mapinduzi
Aidha, Jacqueline Kainja Andrew amesema kuwa, ukarabati wa Ofisi za CCM Urambo uliofanyika sasa ni wa awali kwani ukarabati utaendelea katika hatua zingine zijazo ili kuwa na miundombinu mizuri ya kufanyia kazi za Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Vilevile, viongozi wa Chama na Serikali amempongeza Mbunge Jacqueline Kainja Andrew kwa mchango wake ndani ya Chama hicho na kutoa msisitizo kwa wanachama wengine kuiga mfano wa Jacqueline.Mwisho
Post a Comment