Na Amini Nyaungo
Uchaguzi mkuu wa Tanzania
wa kuchagua Rais,Wabunge,Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka
2025 utakuwepo na utafanyika kama ambavyo ulivyopangwa kwa mujibu wa Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotaka.Hayo ameyasema Mkuu wa
Wilaya ya Manyoni Mhe. Vicent Mashinji (March 10,2025) akiwa moja ya wageni
wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Martha
Gwau alipokuwa anatoa mafunzo kwa Umoja wa Wanawakewa Wilaya ya Manyoni(UWT)
ambapo aliwaleta watalaamu mbalimbali kutoa mafunzo hayo, ambapo DKT. Mashinji ametanabaisha
kuwa uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambao umepangwa kufanyika utakuwepo kama amabavyo ulivyopangwa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.
DKT. Mashinji amesema
katiba inaweka wazi kuwa kila ifikapo miaka mitano na Jumapili ya kila mwisho
ya mwezi Oktoba katika hiyo miaka mitano kunahitajika kufanyike uchaguzi mkuu
na ndivyo ilivyo mwaka huu, hivyo kawaambia wananchi wa Manyoni wasiwe na
wasiwasi kila kitu kitaenda kama kinavyohitajika.
“Naomba niwatoe wasiwasi
uchaguzi mkuu mwaka huu utakuwepo kama kawaida kama katiba inavyosema,
waambieni wakaangalie Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyosema,
hivyo uchaguzi utakuwepo kama kawaida,” DKT. Mashinji.
Tanzania inafanya
uchaguzi kila baada ya miaka mitano kwa ajili ya kuchagua Wabunge, Madiwani
pamoja na Rais.
Mwisho
Post a Comment