TPF NET NA ASKARI MAGEREZA WANAWAKE WATOA MSAADA KWA WAGONJWA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 8, 2025


Na Sylvester Richard

Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF NET) na Askari Magereza Wanawake Mkoa wa Singida wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa wanaopata huduma ya matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mandewa Singida.


Akiongea na wanahabari Mrakibu wa Polisi Brainer John ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Singida amesema kuwa msaada huo una thamani ya zaidi ya Tsh. Millioni 1 na imetolewa kuonesha huruma ya Mama kwa wahitaji ili kuiheshimisha siku ya Wanawake Duniani.

Aidha, Brainer amesema kuwa tangu maadhimisho ya Wanawake  yaanze ngazi ya vijiji hadi kufikia kilele chake tarehe 8 Polisi Wanawake wamekuwa wakijitolea mambo mabalimba ikiwemo utoaji wa elimu ya ukatili wa kijinsia, kuwaona wahitaji mbalimbali na kutoa ushauri kwa wanaofanyiwa ukatili kufika katika ofisi za  madawati ya Jinsia ya Polisi yaliyopo katika Wilaya zote za Mkoa wa Singida ili wapate msaada wa kisheria.
Naye Hashimu Jumanne Mriro ambaye ni Msemaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida amewashukuru askari  wanawake wa Jeshi la Polisi na Magereza kwa majitoleo yao kama Wanawake na kutoa wito kwa watu wengeni kuiga mfano huo  bila kujali kuwa ni Wanawake au Wanaume.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post