Na Amini Nyaungo
Wanawake wamekumbushwa kuyasemea makubwa na mazuri anayoyafanya Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wanachi wake wa Tanzania ambayo yanaonekana na yanaelezeka, wanatakiwa wawe mabalozi wazuri wanakopita.
Hayo ameyasema leo (Marchi 17,2025) Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Martha Nehemia Gwau alipokuwa Iramba katika Baraza la Umoja wa Wanawake la Iramba (UWT) ambalo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Martha ameweka wazi kuwa hivi sasa kila kitu kinaonekana wazi ukiangalia shule, Madawati, Zahanati pamoja na Barabara zinaonekana hivyo wanatakiwa wawe kifua mbele kuyazungunza wala wasione haya.
"Nitumie Baraza hili kuwakumbusha kumsemea vizuri Rais Samia Suluhu Hasani kwa mazuri ambayo anaendelea kuyafanya katika ardhi yetu ya Tanzania, kwahiyo mnapokutana msisahau kumsemea vizuri kwani kila kitu kinaonekana wazi kabisa,"Gwau.
Ametumia fursa hiyo kuwapongeza kina mama wa Iramba kwa utayari wao katika jambo lao kwani amefananisha kama wanajeshi waliotayari vitani akisema kuwa mshikamano huo waende nao hadi mwisho.
"Lakini pia niwapongeze kina mama wa Iramba kwa mshikamano huu, mnaonekana mpo tayari kwa mapambano hongereni sana endeleeni na umoja huu hadi mwisho,"Gwau.
Mheshimiwa Martha Gwau anaendelea na ziara zake kuwatembelea wananchi katika kila wilaya kama ambavyo inavyotakiwa kikanuni akiwa na dhamana ya ubunge.Mwisho.
Post a Comment