Na Amini Nyaungo
Nyota wa Mashujaa FC
inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara Chrispin Ngushi ndiye mfungaji wa goli la
kwanza ligi kuu Tanzania Bara iliyoanza kutimua vumbi Agusti 16,2024 ambapo
yeye amefungo goli hilo tarehe 17.08.2024 Mashujaa walipowafunga Dodoma Jiji 1-0,
katika uwanja wao wa nyumbani wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Ngushi alifunga goli la kufungua pazia la msimu dakika ya 35 ya mchezo
huo na kuandika historia ya kufunga goli la kwanza la mashindano hayo ambapo
bingwa mtetezi klabu ya Yanga yenye maskani yake Twiga na Jangwani pale
Kariakoo Dar es Salaam.
Ngushi aliwahi kucheza
Mbeya kwanza kwa mafanikio makubwa kwa kufunga magoli na kuisaidia timu yake
kupata alama nyingi wakati huo na kusababisha kusajiliwa na Yanga.
Baadae akapata nafasi ya
kucheza Yanga ambapo hakupata nafasi akatolewa kwa mkopo Coastal Union na msimu
huu anautwanga mashujaa
Mchezo wa ufunguzi
Tanzania Prison dhidi ya Pamba uliopigwa tarehe 16. 08.2024 ulitoka sare ya
bila kufungana.
Katika hatua nyingine
raundi ya kwanza yamefungwa magoli 14 mchezo ambao umetoa magoli mengi ni ule
wa Ken Gold dhidi ya Singida Black Stars ambao umetoa magoli 4, Singida
wakiondoka na ushindi wa magoli 3-1 ugenini.
Katika magoli 14 , magoli
saba (7) yamefungwa kipindi cha kwanza huku (7) mengine yamefungwa kipindi cha
pili.
Ligi hiyo kwa sasa ipo
raundi ya 22 na kupitia Chamber Media tutakuandalia magoli yote yaliyofungwa
katika raundi zote.
Mwisho



Post a Comment