By Amini Nyaungo
Mshambuliaji wa Singida Black Stars Jonathan Sowah ameweka wazi
kuwa kiungo wa Yanga Azizi KI moja ya wachezaji bora ndani ya ligi kuu ya soka
ya Tanzania Bara kwakuwa anamjua tangu walipokuwa wanacheza ligi moja nchini
Ghana.
Amesema hayo jana akiwa na Waandishi wa Habari( Media Day)
Singida Black Stars walipokuwa na siku yao ya waandishi wa habari kama bodi ya
ligi inavyoelekeza vilabu vyote viwe na siku maalumu kwa ajili ya waandishi wa
habari kuwauliza mawali wachezaji na viongozi wa imu husika.
Amesema kuwa kama atacheza na Ki atafunga magoli mengi sana
kutokana na ubora wa pasi za mwisho za nyota huyo wa Yanga.
“Azizi Ki ni rafiki yangu tumecheza wote ligi moja nchini Ghana
namjua ni mchezaji mzuri sana kwa ubora aliye nao, kama ningecheza naye timu
moja ingekuwa hatari sana,” Sowa
Pia amesema kuwa ligi ya Tanzania ni nzuri na ina ushindani
sana ana wakaribisha wachezaji wengine waje waone ubora wa ligi hii.
“Nafikiri ni ligi nzuri sana kuna ushindani wa hali ya juu
sana wachezaji wengi waje hapa,” Sowah
Sowah amesema kuwa chakula anachokipenda akiwa nchini
Tanzania ni Wali Maharage au Maharage na Ugali.
“ Chakula kizuri wali na mahaarage au mahaarage na ugali,”
Sowah
Nyota huyo amefunga magoli 7
ya Ligi kuu na amesajiliwa dirisha dogo la ligi bado ligi inaendelea
huenda akafunga mengi Zaidi.
Mwisho


Post a Comment