Na Jumbe Ismaili
![]() |
Kamanda wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya kati,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Bwana Herman Nyanda amesema mradi huo unaotekelezwa katika mfumo wa Ikolojia ya Ruaha-Rungwa umetoa ruzuku hiyo kwa ajili ya kuboresha shughuli za ufugaji na kujikwamua na umaskini pamoja na kupunguza utegemezi wa raslimali za maliasili katika mapori ya Akiba.
Akizungumzia umuhimu wa sekta ya utalii,Kamanda huyo amebainisha kuwa mapori hayo yamekuwa na umuhimu mkubwa kwenye uchumi wa nchi na shughuli za utalii wa uwindaji na utalii wa picha unaofanyika na hivyo kuingizia Taifa fedha za kigeni kila mwaka.
Akifafanua zaidi Kamishina huyo wa TAWA Kanda ya kati amesema kupitia uuzwaji wa vitalu,viingilio,vibali na tozo mbali mbali,katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2022/2023,2023/2024 na 2024/2025 serikali kupitia TAWA Kanda ya kati iliweza kuingiza takribani bilioni 12,657,526,387.60 kupitia shughuli za utalii zinazofanyika katika mapori ya Akiba Rungwa-Kizigo na Muhesi.
Amesema pia kuwa Tawa imekuwa ikisimamia miradi mbali mbali ya maendeleo katika hifadhi za Rungwa-Kizigo na Muhesi inayopitishwa katika bajeti mbali mbali zinazokisiwa na serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na kuidhinishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania..
Kwa mujibu wa Kamanda Nyanda katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha wa 2022/2023,2023/2024 na 2024/2025 serikali kupitia Chama tawala chini ya uongozi wa Raisi Daktari Samia Suluhu Hassan imeweza kutoa shilingi bilioni 1,582,523,012.54/= zilizofanikisha miradi ya ujenzi wa karakana ya kanda ya kati iliyopo makao makuu ya Kanda Manyoni.
Shughuli zingine zilizotekelezwa kupitia fedha hizo ni ujenzi wa uzio wa Makao makuu ya kanda,ujenzi wa ofisi ya makao makuu ya pori la Akiba Muhesi,ujenzi wa kisima na miundombinu ya maji katika pori la Akiba Kizigo,ujenzi wa bwawa na mtandao wa barabara katika pori la Akiba Rungwa.
Hata hivyo kamanda huyo wa TAWA Kanda ya kati amebainisha kwamba Tawa kanda ya kati iliweza pia kufaidika na Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa kupata shilingi milioni 399,012,377.23 ambazo zilitumika katika kuboresha miundombinu ya barabara ya kilomita 42 katika pori la Akiba Rungwa ili kuimarisha shughuli za doria na utalii.
MWISHO.

Post a Comment