VETA SINGIDA KUANZISHA PROGRAM MAALUMU

 Na Amini Nyaungo

Katika kuadhimisha miaka 30 ya Mamlaka ya Chuo cha Ufundi Stadi(VETA) Mkoa wa  Singida kuanzisha program maalumu kwa ajili ya wanafunzi wanaomaliza shule za Msingi na Sekondari kusoma VETA kwa wale watakaohitaji ili waongeze ujuzi.

Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Omary Dendego alipokuwa anafunga katika maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa VETA ambapo Mkoa wa Singida wameadhimisha kuanzia Februari 25 na kutamatika leo (Februari 27,2025).
Dendego amesema kuwa wataandaa program maalumu kwa ajili ya wanaomaliza darasa la saba, Kidato cha Nne na kidato cha Sita wanapomaliza wakati wanasubiria majibu wapate ujuzi kwa miezi sita chuo cha VETA.
Aidha amewaomba wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita na wana mpango wa kuanzisha program wanaomaliza darasa la saba ,kidato cha nne na sita wakati wanasubiri majibu watakaopenda wajiunge na VETA kwa miezi sita.

"Tutaandaa krashi programu kwa ajili ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba, Kidato cha Nne na kidato cha sita watakaotaka waje wajifunze VETA,'' DENDEGO
Amesema kwa mkoa wa Singida shida sio mitaji bali ni ujuzi, huku akiwaunga mkono VETA na vyuo vyote kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Katika hatua nyingine amesema wananchi wanatakiwa waiunge mkono VETA kwa kazi nzuri wanayoifanya pamoja na kuagiza watu wenye ujuzi waendelee na wawatambue wenye ujuzi na wawape ajira ndani ya Halmashauri.

Katika hatua nyingine amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya katika miradi ya Maendeleo hasa kuongeza vyuo vya VETA na sasa kuwa na vyuo vitano kwa mkoa wa Singida.

Halima amepongeza chuo cha VETA hasa  Wakurugenzi kwani vijana wanasoma na kupata ujuzi amesema VETA ni muhimu mno kwani inawawezesha watu wengi kuwa na ujuzi ambao wanaweza kujiajili.


Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post