Na Charles Kikoricho
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amesema kuwa siku ya Mwanamke duniani kimkoa wataenda kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika chuo cha maendeleo ya wananchi FDC .Dendego amesema hayo leo tarehe 1/3/ 2025 ofisini kwake wakati akizungumzia maandalizi ya siku ya Mwanamke kimkoa ambayo itafanyika tarehe 07.03.2025 katika uwanja wa Bombadia.
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa kuanzia leo tarehe 1/3/2025 maadhimisho yameanza katika ngazi ya Vijiji, Kitongoji ,Mitaa,Kata Tarafa na Halmashauri na kuanzia tarehe 5/3/2025 maadhimisho yataanza kufanyika katika ngazi ya Mkoa ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika.
Siku hiyo kutakuwa na michezo mbalimbali katika uwanja wa Bombadia, mpira wa Pete, Ngoma za asili, Muziki wa kizazi kipya, lengo la burudani hizi ni kuhakikisha ujumbe wa siku ya Mwanamke kwa mwaka huu unafika.Lakini pia tarehe 6/3/2025 kutakuwa na kongamano la wanawake wote kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Mkoa na jumla ya wanawake zaidi ya elfu moja watakuwepo katika kongamano hilo kutakuwa na Mada Mbalimbali ambazo zitafundishwa na kujadiliwa kama vile Mwanamke na Uchumi, Nishati safi ya kupikia, Mwanamke na Kodi na uwezeshwaji wa Mwanamke kuwa Mama bora, ukatili.
Tarehe 7/3/2025 itakuwa ndo kilele cha siku ya Mwanamke kimkoa wa Singida ambapo sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa Bombadier ambapo kutakuwa na maandamano ya Wanawake wote na Burudani mbalimbali zitakuwepo katika uwanja wa Bombardier na utoaji wa tuzo kwa Wanawake waliofanya vizuri katika shughuli zao .Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Singida amewaomba wafanyabiashara wasipandishe bei ya bidhaa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na Kwaresma ili wawape nafasi ya waumini kupata unafuu wa kupata mahitaji yao katika kipindi hiki.

Post a Comment