Na Amini Nyaungo
Imeelezwa kuwa binadamu akitumia mazao yaliyoathirika na sumu kuvu anapata madhara makubwa katika afya yake hivyo wameshauriwa wayachambue wakati wa kuvuna ili wasipate madhara yatokanayo sumu kuvu. Hayo ameyazungunza leo Afisa Kilimo Mstaafu wa Wilaya ya Singida Salum Athumani alipokuwa katika kipindi cha asubuhi cha Stanadard Radio akisema kuwa madhara yake ni makubwa na jamiii inatakiwa ijilinde kwa kuyachambua vizuri.
"Sumu kuvu ina madhara makubwa sana kwa walaji inatakiwa kila mmoja ajitahadhari na kuaa makini nayo," Salumu
Aidha alipoulizwa juu ya mkulima atajuaje kama hlzao limeingiwa na sumu kumu, amesema kuwa zao lililoingiwa na ug9njwa huo unaona punje zake zina mavumbi na unabadilika rangi nyingine inakuwa nyeusi huku ladha yake chungu.Aidha katika hatua nyingine Salum ameiomba jamii kuyachagua mazao yao yale yaliyokuwa na ugonjwa huo wayafulie kwani kuna baadhi ya wakulima wanawapa wanyama huku akithibitisha kuwa ukiwapa wanyama na ukimchinja huyo mnyama ukimla unapatwa na madhara ya magonjwa.
"Sio vizuri kumpa mnyama punje zilizokuwa na sumu kuvu maana ukimla unapata magonjwa hayo yatokanayo na Sumu kuvu," Salumu
Katika maelezo yake Salum Athumani amesema kuwa mahindi usivune yakiwa mabichi wakati wa mavuno pia unatakiwa uyatengenezee kichanja kwa ajili ya kuhifadhi.
Wakati wa kufafanua juu ya maana ya sumu kuvu amesema kuwa ni jamii ya fungasi ambayo inapatikana katika mazao, pia huingia katika ardhi, mazao yaliyopata ugonjwa wa Sumu kuvu yanakuwa meusi na machungu akiendelea kusema kuwa Sumu kuvu ni kavumbi tu sio mdudu.
Huku akiweka bayana kuwa mazao yanayoongoza kushambuliwa Mahindi, Mtama na Karanga.
Mwisho.

Post a Comment