SIMBA WARAMBA MILIONI KUMI YA SAMIA

Na Amini Nyaungo
Mabingwa wa zamani ligi kuu Tanzania Bara Simba SC leo wamapokea kitita cha shilingi milioni kumi zawadi ya goli la mama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ambayo ameahidi kuitoa timu za Tanzania zinaposhinda michezo yao katika michuano ya CAF.


Simba wamepata zawadi hiyo baada ya kuibandua CS Costantine mabao 2-0 mchezo uliofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, ambapo magoli ya Simba yakiwekwa kimiani na Kibu Denis dakika ya 61 ya mchezo huku Lionel Ateba akimalizia goli la pili dakika ya 79.



Zawadi hizo zimetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msingwa hii leo.


Simba imetinga hatua ya robo fainali na itakutana na Al Masry ya nchini Misri April mosi na marudio itakuwa April 7.

Post a Comment

Previous Post Next Post