MZIZE, AHOUA NA DUBE WAUANA UFUNGAJI BORA NBC

Na Amini Nyaungo
Ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa katika raundi ya 21 licha ya kuwa na mvuto katika nafasi za juu bado haijulikani nani atakuwa bingwa, moto mwingine unawaka katika mbio za ufungaji bora wa ligi hiyo.


Wachezaji watatu wa Yanga na Simba wamefunga magoli 30 ligi kuu Tanzania Bara.

Clement Mzize amefunga magoli 10 ndani ya ligi kuu Tanzania bara akiwa sawa na mwenzake wa Yanga Prince Dube ambaye amefunga magoli kumi huku Jean Charles Ahoua wa Simba akifunga magoli 10 pia ikiwa ni mchuano mkali kuwania kiatu cha dhahabu.
Wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni pamoja na Lionel Ateba mwenye magoli 8 sambamba na Elvis Rupia aliyetupia magoli 8.


Wengine ni Pacome Zouzou kutoka mabingwa watetezi ligi kuu Tanzania bara aliyefunga magoli 7 sawa na Peter Lwasa kutoka Kagaera Sugar aliyefunga magoli 7.

Katika orodha hii Mtanzania mwingine aliyeingia katika orodha hii ni Paul Peter kutoma Dodoma Jiji mwenye magoli 6.


Swali ambao kila mmoja anajiuliza je wataweza kufikia  rekodi ya msimu uliopita ambapo Azizi Ki amefunga magoli 21 akiwa ndio mfungaji bora.

Post a Comment

Previous Post Next Post