SERIKALI KUONGEZA VYUO 65 VYA VETA

 Na Amini Nyaungo

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongeza kujenga vyuo 65 katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwa na lengo la kuongeza nafasi kwa wanafunzi pamoja na udahili kuongezeka.


Hayo ameyasema leo  Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Ustadi(VETA) CPA Anthony Mzee Kasore alipokuwa katika Ufunguzi wa kilele cha Maadhimisho ya miaka 30 ya VETA Mkoani Singida yaliyofanyika katika Ukumbi wa VETA mkoani hapa.

CPA Kasore amesema kuwa ongezeko hilo la vyuo 65 litaleta tija kwa Watanzania kwani wahitaji watasoma na baadae kupata ajira.


Aidha amesema kuwa kwa sasa kuna vyuo 80 ambapo vinadahili wanafunzi 83,974 kwa mwaka tofauti na ilipoanzishwa ilikuwa na vyuo 14 ambavyo vilikuwa vinadahili wanafunzi 1940.

"Vyuo 65 vinaendelea kujengwa kwenye wilaya mbalimbali nchini ambavyo vinatarajia kuongeza udahili kwa zaidi ya wanafunzi 80,000,"Kasore.


Katika hatua nyingine CPA  Kasore amesema kuwa Sekta za mafunzo zimeongezeka kutoka 10 mwaka 1995 hadi 13 mwaka 2025  ikihusisha fani 89 zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira.

VETA imeanzishwa mwaka 1995 ikiwa na lengo la kuwapatia mafunzo mbalimbali wananchi wa Tanzania ili waweze kujiajiri.


Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post