Charles Kikoricho
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewaomba wanawake wajitokeze kushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu.Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 19.02.2025 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego wakati akizungunza na Standard Radio katika kipindi cha asubuhi cha Zinduka katika kuelekea kilele cha siku ya mwanamke duniani.
Dendego amesema kuwa kujitokeza kwa wanawake katika kushiriki kugombea nafasi za uongozi katika uchagauzi mkuu kutaleta chachu ya maendeleo na kujisimamia wenyewe katika mambo yao na kuongeza haki na usawa katika jamii.
Katika hatua nyingine Dendego amesema kuwa kwa sasa wanawake wamekuwa ni chachu ya kuleta maendeleo hivyo jamii wakiwemo wazee wa kimila na viongozi mbalimbali wawape haki ya kumiliki ardhi kwani wanaouwezo wa kusimamia na kuongoza katika shughuli mbalimbali za maendeleo.Siku ya mwanamke duniani inaadhimishwa tarehe 08,03 ya kila mwaka na kwa mwaka huu siku hiyo kitaifa itafanyika Mkoani Arusha, kwa mkoa wa Singida itaadhimishwa tarehe 07.03.2025 katika uwanja wa Bombadia Manispaa ya Singida na "Kauli mbiu mwaka 'Haki usawa na uwezeshaji''.
Mwisho
Post a Comment