MAZOEZI YA PAMOJA YAIMARISHE USHIRIKIANO KATIKA UTENDAJI

Na Sylvester Richard

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Amon Daudi Kakwale amesema kufanya mazoezi ya pamoja kwa maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kutoka Majeshi ya Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama yazingatiwe ili kuimarisha ushirikiano katika utendaji.
Amebainisha hayo Februari 1, 2025, alipokuwa anazungumza na askari wa Wizara ya Mambo ya Ndani na maafisa TAKUKURU Mkoa wa Singida katika viwanja vya Bombadia Manispaa ya Singida mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya matembezi ya pamoja.
Mazoezi hayo yamefanyika Februari 01, 2025 yakianzia Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Singida kupitia barabara ya Arusha, TRA, Mwenge, Misuna, Barbara ya Dodoma, msalaba mrefu na kumalizika uwanja wa Bombadia.

Post a Comment

Previous Post Next Post