Na Amini Nyaungo
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Jesca Kishoa, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan bungeni Dodoma leo( Januari 31, 2025) wakati wa kuchangia hoja mbalimbali ambapo katika mchango wake, Kishoa alisisitiza maono makubwa ya Rais katika sekta ya nishati na maendeleo ya nchini.Kishao amesema kuwa Tanzania imejaliwa kuwa na Rais mvumilivu na mwenye uwezo wa kuimarisha demokrasia na diplomasia ya uchumi pia alihimiza umuhimu wa kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika Wilaya ya Mkalama.
"Tulinde amani tuliyonayo watu wa usalama wasicheke na mtu anayetaka kuharibu amani ya nchi yetu wanaoumia Wazee, Watoto na wanawake,"Kishoa
Mwisho


Post a Comment