NDULELE AU NDURA au MTULATULA
A: MAJANI YAKE
1.Mwenye ugonjwa wa kisukari chukuwa majani yake, yakaushe kisha ponda ponda upate unga wake na utatumia kwenye maji ya vuguvugu kutwa mara tatu Kwa siku 14 kisha nenda ukapime uje na mrejesho.
2. Kwa mtu anayesumbuliwa na tumbo la hedhi tafuta majani yakaushe ili upate unga wake na kisha tumia kwenye maji moto ni tiba nzuri asubuhi mchana na jioni kikombe cha chai .
3. Mtu mwenye fangasi miguuni atwangetwange majani yake kisha aweke chumvi kiasi chake ,fanya kama unachua au kugulia maeneo yenye fangasi .Hii hutibu mpaka nyungunyungu.
B: MATUNDA YAKE
4. kwa tatizo la mdudu kidoleni, tafuta tunda liloiva la mmea huu, tunda lililoiva toboa weka hicho kidole kutwa nzima, kama hakitosha hakikisha unakamulia mara kwa mara maji yake mdudu atakufa tu. Hapa tunatafuta kuua mdudu yule.
C: MIZIZI YA MTI HUU
5. Kwa tatizo la kuumwa meno au kama jino limetoboka na linakuuma ,basi chukua mzizi wa mti wa huu mbichi au mkavu na kisha chemsha pamoja na chumvi kiasi kisha nyunyizia kwenye shimo au upande wa maumivuau upande wa jino linalouma ,hapa unabunda maji mdomoni kwa dakika 3 hadi 5 kisha unatema fanya mara kadhaaa kisha uache .Fanya hivyo asubuhi mchana na jioni .Hii ni kwa jino lililotoboka na ambalo halijatoboka.Yani kwa jino linalouma
6. Kwa watoto wadogo wa kiume wenye ugonjwa wa ngiri (Hernia ) na au kende (Pumbu) kusinyaa. Basi chukua mizizi ya mti huu na mzizi wa mpapai dume ,mizizi itimie saba kisha Chemsha na umpe anywe kikombe cha chai kutwa Mara mbili kwa siku saba .

Post a Comment