Na Amini Nyaungo
Jamii imetakiwa kuwapa nafasi wanawake katika kumiliki ardhi kwani kufanya hivyo itasaidia kumpa Mwanamke haki na usawa katika Jamii .Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 19.02.2025 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego wakati akizungunza na Standard Radio katika kipindi cha asubuhi cha Zinduka katika kuelekea kilele cha siku ya mwanamke duniani.
Jamii ya Mkoa wa Singida imekuwa na changamoto ya kutokuwapa nafasi wanawake kumiliki mali ikiwemo ardhi ikiamini kwamba mwanamke ni dhaifu hana uwezo wa kusimamia na kumiliki ardhi.Dendego amesema kuwa kwa sasa wanawake wamekuwa ni chachu ya kuleta maendeleo hivyo jamii wakiwemo wazee wa kimila na viongozi mbalimbali wawape haki ya kumiliki ardhi kwani wanaouwezo wa kusimamia na kuongoza katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Siku ya mwanamke duniani inaadhimishwa tarehe 08,03 ya kila mwaka na kwa mwaka huu siku hiyo kitaifa itafanyika Mkoani Arusha, kwa mkoa wa Singida itaadhimishwa tarehe 07.03.2025 katika uwanja wa Bombadia Manispaa ya Singida na "Kauli mbiu mwaka 'Haki usawa na uwezeshaji''.Mwisho
Post a Comment